Kuosha tupu ya nyuma na ya mbele wakati wa kujisafisha

Swali: Wakati mtu anapojisafisha kwa maji ni lazima kuosha tupu ya mbele na ya nyuma au inatosha kuosha tupu ya nyuma peke yake?

Jibu: Ni lazima kuosha tupu ya nyuma na ya mbele pindi kunapotoka uchafu ambao ni kinyesi na mkojo. Kusipotoka kitu na mtu amechengukwa na wudhuu´ kwa sababu ya kutokwa na upepo au kulala au amegusa tupu yake pasi na kizuizi au amekula nyama ya ngamia, basi itatosha kutawadha: ni kuosha uso, mikono miwili kukiwemo viwiko, kupangusa kichwa na masikio na kuosha miguu kukiwemo vifundo viwili vya miguu. Katika hali kama hii ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kujisafisha kwa maji. Kwa sababu hakutokwa na mkojo, kinyesi wala kingine kilicho na hukumu kama viwili hivyo. Akitokwa na mkojo basi inatosha kuosha ncha ya uume wake kutokamana na mkojo. Haikuwekwa katika Shari´ah kuosha tupu ya nyuma ikiwa hakutokwa na kitu. Baada ya hapo atawadhe wudhuu´  wa swalah kama ilivyotangulia. Katika kuosha uso kunaingia vilevile kusukutua na kupalizia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/36)
  • Imechapishwa: 04/08/2021