Swali: Ni ipi hukumu ya kushirikiana na baadhi ya makundi yanayolingania katika Uislamu?

Jibu: Hakuna isipokuwa kundi moja. Makundi na vyama hakuna kheri ndani yake. Amesema (Ta´ala):

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.”[1]

Kuna kundi moja; nao si wengine ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hakuna wengine walio juu ya haki mbali na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tunazungumzia haki isiyokuwa na utata ndani yake. Makundi mengine yana makosa na upotevu. Lakini hata hivyo hayako sawa. Yapo ambayo yako karibu na yako ambayo yako mbali. Katika Uislamu hakuna makundi. Hakuna isipokuwa kundi moja tu:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane. Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu pindi mlipokuwa maadui halafu akaunganisha kati ya nyoyo zenu.”

[1] 03:103

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 25/11/2018