Inatakiwa kula tende kwa kuwitiri kabla ya kwenda katika uwanja wa ´Iyd


Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kwenda katika ´Iyd-ul-Fitwr alikuwa akila tende kwa kuwitiri. Je, kuna kikomo cha witiri hiyo na kunaingia vilevile tende tatu, tano, saba, tisa kumi na moja na kadhalika?

Jibu: Hakuna kikomo cha witiri kinachotakikana juu ya wingi. Lakini isiwe chini ya tende tatu kwa sababu ndio kiwango cha chini. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/234)
  • Imechapishwa: 14/06/2018