Swali: Sisi tuko mbali na msikiti kwa 4 km na wala hatusikii adhaana ingawa tuko na Khatwiyb anayeishi pamoja nasi. Ni ipi idadi ya chini ya waswaliji ili isihi swalah ya ijumaa?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana maoni mbalimbali juu ya idadi ya kusihi kwa swalah ya ijumaa. Maoni yaliyo na nguvu na ya sawa zaidi ni kwamba watu watatu wanatosha na kwamba swalah inaweza kuswaliwa kwa idadi hiyo. Swalah itawalazimikia muda wa kuwa ni wakazi na waungwana. Ama wakiwa watatu, kumi au zaidi ya hapo watatakiwa kuswali swalah ya ijumaa kwa sababu mnaishi mbali na msikiti kunakoswaliwa ijumaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/14270/%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%AF%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%8A-%D8%AA%D9%82%D8%A7%D9%85-%D8%A8%D9%87-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9
  • Imechapishwa: 15/05/2020