as-Suhaymiy kuhusu Wahdat-ul-Wujuud na Khaalid ar-Raashid


Swali: Je, katika shairi hili kuna kosa la ´Aqiydah: ”Allaah ndio Mola Wangu. Sitaki mwingine asiyekuwa Yeye. Je, hivi uwepeo wa uhakika wa mwingine kuliko Yake?”?

Jibu: Bali kuna kosa la ´Aqiydah ambalo ni khatari sana. Azinduliwe msemaji wa shairi hili. Kwa kuwa huenda hakufahamu maana yake inayoashiriwa au inayokusudiwa. Neno lake “Je, hivi uwepeo wa uhakika wa mwingine kuliko Yake” – hii ndio kauli ya Wahdat-ul-Wujuud. Ndio ´Aqiydah ya Ibn ´Arabiy, Ibn Faariyd, Ibn Sab´iyn, al-Faaraabiy na wengineo waliokuwa na ´Aqiydah Wahdat-ul-Wujuud.

Wanasema kuwa mja ndio Mola na Mola ndio mja na kwamba hakuna uhakika wa kuwepo isipokuwa uwepo wa Allaah (´Azza wa Jalla). Kila unachoshuhudia, unachokiona, unachokihisi, unachokionja na unachokigusa ni Allaah (´Azza wa Jalla).

Kuna mmoja leo katika wananadharai mwandishi mjinga kaandika hilo katika Suurat-ul-Ikhlaasw. Katika tafsiri yake inayoitwa “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”. Kadhalika katika Kauli Yake Allaah (´Azza wa Jalla):

قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ

“Sema: “Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema : “Allaah ndiye shahidi baina yangu na baina yenu.”” (06:19)

Kauli hii ni mbaya tena khatari zaidi kuliko kauli ya Fir´awn pale aliposema:

أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni Mola wenu mkuu.” (79:24)

Hali kadhalika Ibn ´Arabiy amesema kuwa Fir´awn alikuwa ameongoka zaidi kuliko Muusa wakati aliposema:

أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni Mola wenu mkuu.” (79:24)

Kwa kuwa Fir´awn alikuwa ametambua uhakika ambao Muusa (´alayhis-Salaam) alikuwa hakuutambua.

Wanaoamini Wahdat-ul-Wujuud wanapatikana mpaka hii leo. Mmoja wao wao ni Mustwafa Mahmuud ambaye anasema siku zote kwamba kila kinachoonekana ni Allaah. Baadhi ya watu wanadanganyika naye. Tunatakiwa kuwa makini juu ya hili.

Aliyesema hivi, au kusema shairi hili, afundishwe na akumbushwe. Aidha ajirudi na la sivyo atakuwa ni mmoja katika wale ambao wako na ´Aqiydah hii – na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=v5pRojlo4-E
  • Imechapishwa: 27/01/2018