Anataka kulipiza kisasi kwa mkono wake kwa aliyemuua nduguye

Swali: Sisi ni vijana ambao tumebishana juu ya masuala miongoni mwa masuala ya kisasi. Ni ipi hukumu endapo mtu atauliwa na huyo muuliwaji yuko na ndugu yake ambaye akamakinishwa juu ya yule muuaji ambapo akamuua papo hapo. Je, anapata dhambi? Je, kwa kitendo hicho anakuwa amelipiza juu ya nduguye? Je, kitendo hichi kinaingia ndani ya maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Mtapata katika kisasi uhai, enyi wenye akili, ili mpate kumcha Allaah.”[1]

Jibu: Haijuzu kwa ndugu wa aliyeuliwa kufanya haraka kumuua muuaji. Bali ni lazima kufanya subira na kutofanya haraka mpaka kwanza kutazamwa sababu ya kuua na mpaka warithi wakusanyike juu ya kuomba kisasi au kusamehe. Haijuzu kwake kufanya haraka katika mambo haya. Kwa sababu kunaweza kuwa sababu zinazozuia kulipiza kisasi. Kwa hiyo ni lazima kwa yule aliyefikwa na mtihani huyo asifanye haraka na alipeleke mashtaka kwa watawala ili kisasi kitazamwa kwa mujibu wa Shari´ah. Kuhusu kufanya haraka kunaweza kumpelekea katika yale aliyoharamisha Allaah.

Mwendesha kipindi: Kwa hiyo kisasi hakiko mikononi mwao?

Ibn Baaz: Kisasi kiko mikononi mwa warithi wote maoni yao yakikusanyika juu ya kisasi na muuaji akawa ni mwenye kustahiki jambo hilo. Lakini kukiwa kuna vikwazo basi ni lazima hakimu wa Kishari´ah alitazame jambo hilo.

Mwendesha kipindi: Ni nani anayesimamisha kisasi wakimwacha?

Ibn Baaz: Atakisimamisha hakimu wa Kishari´ah kupitia kwa watawala.

[1] 02:179

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28605/%D8%A8%D8%B9%D8%B6-%D8%A7%D8%AD%D9%83%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B5%D8%A7%D8%B5
  • Imechapishwa: 14/02/2020