al-Waadi´iy kuoa kwa nia ya kuacha


Swali 373: Ni ipi hukumu kuhusu ndoa kwa nia ya kuacha?

Jibu: Haya nimeyapata kwenye fatwa ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na anasema akimuoa mwanamke kisha wakati anaporejea kutoka katika mji ule akamwacha ndoa hiyo imechukizwa. Kwani imefanana na Mut´ah. Kinachonidhihirikia ni kwamba muislamu anatakiwa kujiepusha nayo kwa sababu isije kuwa ni aina fulani ya Mut´ah. Kwani ndoa hiyo imekaribia maana ya Mut´ah. Rejeeni masuala hayo katika “Majmuu´-ul-Fataawaa” ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika mjeledi maalum unaozungumzia ndoa. Kimbilia kujiepusha na mambo yenye utata.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 627
  • Imechapishwa: 08/12/2019