88. Ni wajibu kuhukumu kwa aliyoteremsha Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Hapana kulazimisha katika dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Hivyo basi, yule atakayemkanusha waungu wa batili na akamwamini Allaah, kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote. Mjuzi wa kila kitu.” (al-Baqarah 02 : 256)

MAELEZO

Hii ndio maana ya “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”.

Dalili – Bi maana dalili juu ya ulazima wa kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah na kukanusha kufuru.

“Hapana kulazimisha katika dini… – Hapana kulazimishana katika dini kutokana na kudhihiri dalili zake na kuwa kwake wazi. Ndio maana akasema:

قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ

“Kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu.”

Ikiwa uongofu umekwishabainika kutokamana na upotofu, basi ni lazima kwa kila nafsi iliyosalama kuchagua uongofu badala ya upotofu.

“Basi atakayemkanusha twaaghuut na akamwamini Allaah… – Allaah (´Azza wa Jall) ametaja mtu kuanza kukanusha kufuru kabla ya kumwamini Allaah. Kwa sababu kutimia kwa mambo kunakuwa pale ambapo vizuizi vyote vinaondoshwa kabla ya kupatikana kinachothibishwa.

“Kwa hakika atakuwa ameshikilia barabara kishikilio madhubuti” – Bi maana atakuwa ameshikilia kishikilio madhubuti. Kishikilio madhubuti ni Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 159-160
  • Imechapishwa: 05/06/2020