83. Ndio maana makafiri watazuiwa siku ya Qiyaamah


Kuhusu makafiri, kwa vile walimkufuru na wakakadhibisha alama Zake duniani, basi Allaah atajizuia nao wasimuone siku ya Qiyaamah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Sivyo hivyo! Hakika wao Siku hiyo bila shaka watazuiwa wasimuone Mola wao.”[1]

Bi maana siku ya Qiyaamah. Kwa ajili ya kuwatweza hawatomuona Mola wao. Kwa sababu wamemkanusha na wakamkufuru duniani, basi Allaah atawanyima kumuona siku ya Qiyaamah.

[1] 83:15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 62
  • Imechapishwa: 18/08/2021