44. Yuko juu ya ´Arshi na anajua kila kitu


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Yeye yuko juu ya ´Arshi Yake kwa utukufu na kwa dhati Yake na yuko kila mahali kwa ujuzi Wake.

MAELEZO

Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake kwa dhati Yake na si kwa ujuzi Wake, kama wanavodai Mu´awwilah wanaposema kuwa Allaah yuko juu kwa ujuzi, uwezo au utawala Wake. Uhakika wa mambo ni kwamba Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu kwa dhati Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ‘Arshi.”[1]

Kulingana ni sifa ya kimatendo tofauti na ujuu ambayo ni sifa ya kidhati. Ndio maana kulingana kukatajwa sambamba na kuumba mbingu na ardhi. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”

Kwa hivyo kulingana ni sifa ya kimatendo ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) husifiwa kwayo pale anapotaka, ilihali ujuu ni sifa ya kidhati ambayo daima anasifiwa kwayo. Sentesi:

اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… akalingana juu ya ´Arshi.”[2]

imetajwa sehemu saba ndani ya Qur-aan na daima hutajwa namna hiyo. Hii inajulisha kuwa maana yake ni moja, nako ni kuwa juu na kungatika juu ya ´Arshi. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Wana maana nne juu yake:

kuthibiti, kuwa juu na kungatika

Hayakanushwi;

kupanda ambako ndio maana ya nne

Tafsiri hiyo imechaguliwa na Abu ´Ubayd, mwanafunzi wa ash-Shaybaaniy

kwani yeye ni mtambuzi zaidi wa Qur-aan kuliko Jahmiy

Wao, tofauti na Mu´attwilah, wana tafsiri nne juu ya neno (الإستواء): kuthibiti, kuwa juu, kungatika na kupanda. Jahmiyyah wanapinga ujuu na kulingana na wanasema kuwa Allaah yuko kila mahali kukiwemo sehemu za taka na vyoo – Allaah ametakasika kutokamana na hayo!

Mshairi amesema:

“… kwa dhati Yake… “

Hapa wanaraddiwa Mu´awwilah kama vile Ashaa´irah na wengineo wanaosema kuwa (الإستواء) maana yake ni kutawala juu ya ´Arshi.

Licha ya kuwa Allaah yuko juu ya viumbe ujuzi Wake uko kila mahali. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ

“Hakika Allaah hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.”[3]

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

“Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”[4]

Bi maana kwa ujuzi Wake.

Yuko juu ya viumbe Wake kwa dhati Yake

na hakuna maeneo ardhini inakosekana elimu Yake

[1] 20:5

[2] 7:54

[3] 3:5

[4] 57:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 28/07/2021