40. Ni ipi hukumu kwa anayeonelea kuwa katika Uislamu kuna vitu vidogo vidogo na kuvidharau?


Swali 40: Unasemaje kwa ambaye anasema kuwa katika dini ya Uislamu kuna mambo ya misingi na ya matawi?

Jibu: Katika dini ya Uislamu kuna mambo ya msingi yenye kuzingatiwa. Nayo si mengine ni ´Aqiydah. Vilevile kuna mambo ya matawi kwa mtazamo wa zile hukumu za vitaga ambazo ni za ki-Fiqh katika ´ibaadah na mambo ya matangamano. Kwa mtazamo kama huu ni sawa.

Ama mwenye kusema kuwa katika Uislamu kuna mambo ya msingi na mambo madogo madogo, hili ni kosa la fedheha. Uislamu wote ni mambo ya msingi. Hakuna mambo madogo madogo. Uislamu wote ni haki na hakuna batili ndani yake. Uislamu wote ni mambo yenye kukusudiwa kweli na si ya mchezo. Anayedai kuwa katika Uislamu kuna mambo ya msingi na madogo madogo, hakika huyu ni dhalimu na mvuka mipaka. Kunakhofiwa juu yake akawa amehukumiwa kuritadi kwa sababu ya maneno haya.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017