23. Msafara wa kwanza wa kijeshi Badr


Baada ya takriban siku kumi akatoka tena kwenda katika msafara wa kijeshi kwenda Badr. Kikosi hicho kilitokamana na kwamba Kurz bin Jaabir al-Fihriy alikuwa ameshambulia kundi huko al-Madiynah wakati lilikuwa nje na kulisha wanyama wao. Wakamtafuta mpaka walipofika katika bonde linaloitwa Swafawaan lilioko pembezoni mwa Badr. Kurz akawa amefanikiwa kukimbia na kikosi kikarudi. Wakati huo alikuwa amemfanya Zayd bin Haarith (Radhiya Allaahu ´anh) kubaki khalifa al-Madiynah.

Inasemekana vilevile kwamba alimtuma Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) kwenda kumtafuta Kurz bin Jaabir na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Imesemekana vilevile kuwa alimtuma juu ya jambo lingine.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 43
  • Imechapishwa: 26/04/2018