17. Tanbihi ya kwanza katika al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar


Tanbihi ya kwanza ni kuwa ni katika mfumo wa Salaf kusema “´alayhis-Swalaatu was-Salaam” au “Swalla Allaahu ´alayhi wa salam” wakati Mtume wa Allaah au Mtume mwingine anapotajwa.

Wakati Swahabah anapotajwa kunasemwa “Radhiya Allaahu ´anhu”. Hawatofautishi kati yao hata kama fadhila zao zinatofautiana.

Ama kuhusu Shiy´ah, hutoona jengine zaidi ya matusi na ukufurishaji na wakati mwingine laana pindi Swahabah anapotajwa. Isipokuwa tu idadi chache kama Abu Dharr na al-Muqdaad. Hapo ndipo husema “Rahimahu Allaah”.

Wakati ´Aliy anapotajwa husema “´alayhis-Salaam”. Husema hivo vilevile wakati mmoja katika maimamu wao kumi na mbili anapotajwa. Wameshikamana na hilo bara bara mpaka imekuwa ni moja katika alama zao.

Mimi siwapaki mafuta. Wakati ´Aliy anapotajwa ninasema “Radhiya Allaahu ´anhu” kama inavofanywa kwa ndugu zake watukufu wengine katika Maswahabah. Pindi imamu miongoni mwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotajwa ninasema “Rahimahu Allaahu”. Haijalishi kitu hata kama Raafidhwah wanasema “´alayhis-Salaam”. Sintowapaka mafuta katika kupetuka kwao mipaka na alama yao. Bali ninatangamana na maimamu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama wanachuoni wengine wote wa Kiislamu, watu waheshimiwa na waislamu wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 19/03/2017