17. Majina mawili yanayopendwa zaidi na Allaah


Majina yaliyopendekezwa na kujuzu yamegawanyika katika ngazi mbalimbali na yako kama ifuatavyo:

1- Imependekezwa kumpa mvulana jina la “´Abdullaah”, mja wa Allaah, au “´Abdur-Rahmaan”, mja wa Mwingi wa rehema. Hayo ndio majina yanayopendwa zaidi na Allaah (Ta´ala), kama ilivyothibiti ikiwa ni pamoja vilevile na Muslim na Abu Daawuud kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Majina hayo mawili yanathibitisha uja ambao ndio uhakika wa mwanaadamu. Allaah ametaja tu majina hayo mawili pindi alipokuwa akitilia mkazo uja wa mwanaadamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا

“Pindi mja wa Allaah aliposimama kumwomba walikaribia kumzonga [kama vile wanataka kumwacha].” (72:19)

وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا

“Waja wa Mwingi wa Rahmah ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu.” (25:63)

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖأَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ

“Sema: “Muiteni Allaah au muiteni Mwingi wa Rahmah! Vyovyote mtakavyomwita [bado ni Yule Yule Mmoja], Yeye ana majina Mazuri kabisa.” (17:110)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa binadamu yake jina la “´Abdullaah” (Radhiya Allaahu ´anh).

Kulikuwa takriban Maswahabah 300 wakiitwa “´Abdullaah”. Mtoto wa kwanza wa Muhaajiruun aliyezaliwa alipewa jina la “´Abdullaah”, naye ni ´Abdullaah bin az-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 16
  • Imechapishwa: 18/03/2017