14. Mwanamke anaruhusiwa kuonesha uso mtumwa wake


5- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ikiwa mmoja wenu [wanawake] ana mtumwa mwenye kulipa kwa ajili ya kutaka kujiacha huru, basi ajisitiri mbele yake.”[1]

Imepokelewa na watano isipokuwa ni an-Nisaa´iy na ni Swahiyh kwa mujibhu wa at-Tirmidhiy.

Chenye kulengwa katika Hadiyth hii kwamba mmiliki mwanamke anaruhusiwa kuonesha uso wake kwa mtumwa wake midhali bado anammiliki. Pale tu ambapo anakuwa huru basi ni wajibu kwake kujisitiri kwa sababu mtumwa huyo amekuwa ni ajinabi kwake. Ni dalili yenye kuonesha kuwa mwanamke ni wajibu kujifunika mbele ya mwanaume ajinabi.

[1] Ahmad (27006), Abu Daawuud (3928), at-Tirmidhiy (1261) na Ibn Maajah (2520).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 19
  • Imechapishwa: 26/03/2017