04 – Madhambi yanapelekea kuhisi upweke na watu

Madhambi yanapelekea katika upweke ambao unakuwa kati ya yule mtenda dhambi na watu na khaswa khaswa wale watu wema. Anahisi upweke kati yake yeye na wao. Kadri na jinsi anavyohisi upweke ndivyo anavyokuwa mbali na wao na vikao vyao, ananyimwa baraka za kufaidika na wao na analikurubia kundi la shaytwaan kiasi na atavyokuwa mbali na kundi la Allaah. Upweke huu huwa mkubwa mpaka unashinda na kuchukua nafasi kati yake yeye na mke wake, mtoto wake, ndugu zake na yeye mwenyewe. Ndio maana utamuona anavyohisi ugeni juu ya nafsi yake mwenyewe. Baadhi ya Salaf wamesema:

“Pindi ninapomuasi Allaah basi huyaona hayo katika tabia ya mnyama wangu na mke wangu.”

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 66
  • Imechapishwa: 30/12/2017