Zipu zinazokuwa nyuma kwenye mavazi ya wanawake

Swali: Baadhi ya wanawake wanavaa nguo zenye zipu nyuma yake. Je, hili linajuzu?

Jibu: Hatuwezi kukataza, hatujui tatizo lolote katika hilo. Lakini ikiwa zipu itakuwa mbele ni bora zaidi na ni yenye kuhifadhi zaidi sehemu za siri. Kilicho muhimu ni kuhifadhi sehemu ya siri. Istilahi hii mpya si nzuri. Ikiwa zipu ingekuwa mbele ingekuwa bora zaidi na yenye tahadhari zaidi. Ikiwa mbele yake, anaweza kuihifadhi na kuilinda. Kwa hivyo ni bora kuliko nyuma. Lakini ikiwa ipo nyuma na haioneshi sehemu ya siri, inalinda na imewekwa kwa sababu ya urahisi wa kuvua nguo au sababu nyingine, basi hatuoni tatizo ndani yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1098/حكم-وضع-النساء-سحابات-من-خلف-ثيابهن
  • Imechapishwa: 15/12/2025