Zakaah ya ngamia ambao wanachungwa shambani au porini

Swali: Nimenunua kundi la ngamia ishirini ambao nikawaweka katika shamba langu. Zakaah yao itakuwaje iwapo mwaka utawapitia?

Jibu: Ngamia, kondoo na ng’ombe kuhusu zakaah yao ni sharti wawe wanachungwa porini. Ama ikiwa mtu anawalisha nyumbani kwake au katika shamba lake, basi hakuna zakaah juu yao. Zakaah ipo kwa wale wanaochungwa katika sehemu kubwa ya mwaka au mwaka wote. Ikiwa katika sehemu kubwa ya mwaka au mwaka wote wanapewa chakula, hakuna zakaah juu yao, si kwa ngamia, ng’ombe wala kondoo.

Swali: Je, hawa si hawahesabiwi kuwa ni bidhaa za biashara?

Jibu: Isipokuwa ikiwa alikusudia biashara, basi ndiyo. Ikiwa alikusudia biashara, basi zakaah yao inakuwa ni Zakaah ya mali ya biashara. Atatoa zakaah yao kama zakaah ya biashara pindi mwaka utakapowapitia. Atatoa Zakaah ya thamani yao, si idadi ya vichwa vyao. Atatoa zakaah ya thamani yao, kwa sababu wakati huo zinahesabiwa kuwa ni bidhaa za biashara, hata kama anawalisha nyumbani kwake au katika shamba lake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2242/حكم-الزكاة-في-الانعام-غير-الساىمة
  • Imechapishwa: 05/03/2026