Swali: Nina watoto mayatima, nami ni ami yao tunaishi nyumba moja. Ninawahimiza kudumu katika swalah, lakini katika swalah ya Fajr hawaswali pamoja na mkusanyiko, bali huiswali asubuhi. Nifanye nini? Niwafukuze nyumbani au nifanye nini hali ya kuwa hawana mwingine isipokuwa mimi?
Jibu: Ni juu yako kusimamia malezi yao hata kwa kuwatia adabu kwa kupiga mpaka warekebike na waswali Fajr pamoja na mkusanyiko. Usiwafanyie wepesi, wakiasi, basi wafukuze ikiwa wamefikia umri wa kuwajibika ´ibaadah. Wafukuze kwa maslahi ya nafsi zao. Usiwafanyie wepesi kabisa. Ukiweza kuwatia adabu kwa kupiga basi wapige mpaka warekebike na waswali pamoja na wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”[1]
Ikiwa wamebaleghe, basi jambo lao ni kubwa zaidi. Wanastahiki kuamrishwa watubie, kwani anayeswali swalah baada ya kuchomoza jua hakuiswali. Ni lazima aiswali katika wakati wake. Aidha ni lazima aiswali pamoja na mkusanyiko msikitini. Haijuzu kulegeza mambo kwa hawa, ni mamoja wawe ni watoto wako, watoto wa ndugu yako au mtu yeyote aliye chini ya uangalizi wako.
[1] Abu Daawuud (495). Hadiyth ni Swahiyh. Tazama ”Nasb-ur-Raayah” (1/298) kwa tamko kama hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/206)
- Imechapishwa: 25/02/2026
Swali: Nina watoto mayatima, nami ni ami yao tunaishi nyumba moja. Ninawahimiza kudumu katika swalah, lakini katika swalah ya Fajr hawaswali pamoja na mkusanyiko, bali huiswali asubuhi. Nifanye nini? Niwafukuze nyumbani au nifanye nini hali ya kuwa hawana mwingine isipokuwa mimi?
Jibu: Ni juu yako kusimamia malezi yao hata kwa kuwatia adabu kwa kupiga mpaka warekebike na waswali Fajr pamoja na mkusanyiko. Usiwafanyie wepesi, wakiasi, basi wafukuze ikiwa wamefikia umri wa kuwajibika ´ibaadah. Wafukuze kwa maslahi ya nafsi zao. Usiwafanyie wepesi kabisa. Ukiweza kuwatia adabu kwa kupiga basi wapige mpaka warekebike na waswali pamoja na wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”[1]
Ikiwa wamebaleghe, basi jambo lao ni kubwa zaidi. Wanastahiki kuamrishwa watubie, kwani anayeswali swalah baada ya kuchomoza jua hakuiswali. Ni lazima aiswali katika wakati wake. Aidha ni lazima aiswali pamoja na mkusanyiko msikitini. Haijuzu kulegeza mambo kwa hawa, ni mamoja wawe ni watoto wako, watoto wa ndugu yako au mtu yeyote aliye chini ya uangalizi wako.
[1] Abu Daawuud (495). Hadiyth ni Swahiyh. Tazama ”Nasb-ur-Raayah” (1/298) kwa tamko kama hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/206)
Imechapishwa: 25/02/2026
https://firqatunnajia.com/watoto-mayatima-wanaochukulia-wepesi-swalah-ya-fajr/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket