Swali: Je, watoto wa kiume na wa kike wanapata ujira wakimfundisha baba yao mzee swalah?
Jibu: Ni wajibu wao kumfundisha ikiwa hajui. Lakini wafanye hivyo kwa upole, huruma na maneno mazuri, si kwa ukali, ili awakubalie. Hali kadhalika kwa wazee wengine, yule anayefundisha anatakiwa kutafuta upole, kwa sababu kufanya hivo ni rahisi zaidi kukubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Anayenyimwa upole, basi hunyimwa kheri yote.”[1]
Kwa hiyo mtoto akiwa na baba yake, kaka yake mkubwa, babu yake au mama yake, anatakiwa kuwa mpole sana kwao ili wapokee mawaidha yake. Vivyo hivyo kwa wengine, kwa sababu ukali unaweza kusababisha kukataliwa na kutopatikana kwa manufaa.
[1] Muslim (2592).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/209)
- Imechapishwa: 25/02/2026
Swali: Je, watoto wa kiume na wa kike wanapata ujira wakimfundisha baba yao mzee swalah?
Jibu: Ni wajibu wao kumfundisha ikiwa hajui. Lakini wafanye hivyo kwa upole, huruma na maneno mazuri, si kwa ukali, ili awakubalie. Hali kadhalika kwa wazee wengine, yule anayefundisha anatakiwa kutafuta upole, kwa sababu kufanya hivo ni rahisi zaidi kukubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Anayenyimwa upole, basi hunyimwa kheri yote.”[1]
Kwa hiyo mtoto akiwa na baba yake, kaka yake mkubwa, babu yake au mama yake, anatakiwa kuwa mpole sana kwao ili wapokee mawaidha yake. Vivyo hivyo kwa wengine, kwa sababu ukali unaweza kusababisha kukataliwa na kutopatikana kwa manufaa.
[1] Muslim (2592).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/209)
Imechapishwa: 25/02/2026
https://firqatunnajia.com/watoto-kumfunza-mzazi-wao-swalah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket