Wanazuoni kutumia fursa ya vyombo vya khabari katika kueneza dini

Swali: Ni ipi maoni yenu kuhusu kutochukua hatua kwa wanazuoni, maneno yao kutokuwa katika vyombo vya khabari, kutowaelekeza waislamu na pia kutengwa kwa wanazuoni na watawala?

Jibu: Yote haya ni kama ilivyotangulia. Ni wajibu juu ya mwanachuoni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake. Kwa hakika mengi tayari yamefanyika. Wanazuoni wengi wamefafanua, wameweka wazi, wameandika na wameeleza kupitia redio, TV na magazeti. Wamebainisha mambo mengi. Lakini ni nani anayenufaika? Si wengi miongoni mwa watu wa kawaida wala wasomi. Hata hivyo bado haijafikia kiwango kamili kinachotakiwa. Haja bado ipo ya kufanya zaidi. Tunawahimiza wanachuoni wengine waliobaki nao wasimame pia kidete. Mambo haya ni katika faradhi ya kutoshelezana; yakitekelezwa na idadi inayotosha katika kubainisha haki, basi inatosha. Lakini kadiri wanazuoni wanavyoongezeka na wanavyofuatana katika kila mahali katika kuwalingania watu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), basi hilo litakuwa na manufaa zaidi kwa watu na litakuwa kamilifu zaidi katika kuwaongoza na kuwaamsha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1399/دعوة-للعلماء-باستغلال-وساىل-الاعلام-لنشر-العلم
  • Imechapishwa: 05/04/2026