Waislamu kuwa na umoja katika kupambana na maadui

Swali: Nimesoma makala ya mmoja wa wanazuoni akisema kuwa yale yanayowapata waislamu ya kutawaliwa na maadui na kuvamiwa kwa maeneo yao matukufu ni faradhi ya kila muislamu kuwatetea dhidi ya dhuluma hiyo. Je, ni ipi maoni yenu kuhusu hilo?

Jibu: Imeshatangulia maneno kuhusu jambo hili. Wajibu juu ya waislamu ni kushikamana pamoja na kushirikiana dhidi ya maadui zao ili kuzikomboa nchi zao kutoka mikononi mwa mayahudi na wengineo. Ni lazima waislamu washikamane na washirikiane kupambana jihaad dhidi ya maadui wa Allaah kwa ajili ya kuzikomboa nchi zilizo chini ya udhibiti wa mayahudi, na kwa ajili ya kupigana na kila aliyejitenga na dini ya Allaah na asiyetawala kwa Shari´ah ya Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1393/واجب-المسلمين-في-الدفاع-عن-دينهم-وارضهم
  • Imechapishwa: 05/04/2026