Swali: Anaomba mtukufu awatahadharishe watu kuhusu kukatazwa kupita mbele ya waswaliji katika swalah?
Jibu: Kupita mbele ya anayeswali ni jambo lisilojuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau mmoja wenu angesimama miaka arobaini ingekuwa bora kwake kuliko kupita mbele ya anayeswali.”
Amekataza kupita mbele ya anayeswali na akaamrisha kumzuia anayepita mbele ya anayeswali. Hivyo haijuzu kwa muislamu kupita mbele ya ndugu yake ikiwa anaswali. Hapa ni pale ambapo akiwa ni imamu, anaswali peke yake na yuko karibu naye. Ama ikiwa ni maamuma haidhuru, kwa sababu maamuma inamtoshea Sutrah ya imamu wake, hata wakipita mbele ya maamuma haidhuru. Kuhusu imamu, hapaswi kupitiwa mbele yake wala kati yake na Sutrah yake. Vivyo hivyo anayeswali peke yake, hapaswi mtu kupita mbele yake wala kati yake na Sutrah yake. Lakini ikiwa mtu yuko mbali naye au anapita nyuma ya Sutrah, hakuna ubaya. Ikiwa ana Sutrah kama fimbo iliyochomekwa, kiti au kitu kingine kama nguzo na mtu akapita nyuma yake, haidhuru. Kadhalika ikiwa amepita mbali naye zaidi ya dhiraa tatu, basi hilo halimdhuru.
Kuhusu katika msikiti Mtakatifu haidhuru, kwa sababu ni vigumu kujiepusha na hilo.
Unapitaji unaobatilisha swalah ni pale ambapo mpitaji ni mwanamke, punda au mbwa mweusi; vitu vitatu vikapita mbele ya anayeswali kati yake na Sutrah au ndani ya umbali wa chini ya dhiraa tatu, basi swalah yake inabatilika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kinakata swalah ya muislamu ikiwa hana mbele yake kitu kama sehemu ya nyuma ya tandiko: mwanamke, punda na mbwa mweusi.”
Lakini ikiwa anayepita ni mwanaume au mnyama mwingine asiye mbwa mweusi kama ngamia, kondoo au mbwa asiye mweusi, hakibatilishi swalah. Lakini hupunguza ukamilifu wake. Haifai kupita. Inapaswa azuiwe anayepita. Mtoto mdogo pia azuiwe, lakini hakibatilishi.
Urefu wa Sutrah ni takriban thuluthi mbili ya dhiraa, karibu nusu mita kutoka ardhini.
Katika msikiti Mtakatifu ndani ya Ka‘bah, kupita hakikatishi swalah kwa sababu hili haliwezi kuzuiwa. Isitoshe Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakuwa wakizuia kupita ndani yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3508/حكم-المرور-بين-يدي-المصلين
- Imechapishwa: 24/11/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3508/حكم-المرور-بين-يدي-المصلين
Imechapishwa: 24/11/2026
https://firqatunnajia.com/usipite-mbele-ya-anayeswali/