Ulazima wa kumfata imamu katika swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya baadhi ya wanawake ambao hawaswali nyuma ya imamu kama inavyopasa, bali wanarukuu na kusujudu wanavyotaka wao?

Jibu: Hili halijuzu. Swalah yao huwa batili. Anayeswali nyuma ya imamu ni lazima amfuate imamu wala asimtangulie. Hafai kufanya mchezo, ni mamoja awe mwanamume au mwanamke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika imamu amewekwa ili afuatwe. Msitofautiane naye. Kwa hiyo akisema:

الله أكبر

”Allaah ni Mkubwa.”

nanyi semeni:

الله أكبر

”Allaah ni Mkubwa.”

Wala msilete Takbiyr mpaka yeye kwanza alete Takbiyr. Akienda katika Rukuu´, nendeni katika Rukuu´… ”[1]

Kwa hiyo ni lazima kumfuata imamu na haijuzu kufanya mchezo.

[1] Sunan Abiy Daawuud (857) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/144)
  • Imechapishwa: 05/03/2026