Swali: Kuna misikiti iliyojengwa kwa umbo la duara kama mpira, kiasi kwamba safu ya kwanza huwa ndogo, ya pili huwa kubwa zaidi na safu zinaendelea kuongezeka kisha za mwisho hurudi kuwa kama za mwanzo. Je, mtindo huu wa ujenzi unajuzu kwa upande wa misikiti?

Jibu: Sijui kuwa kuna dalili maalum juu ya mtindo huu. Kinalopaswa ni misikiti iwe pana na iliyo sawa ili safu ziwe zimenyooka na zilizolingana. Hili ni bora zaidi kwa sababu ni pana zaidi kwa wanaoswali na lina manufaa zaidi kwa watu wa eneo husika. Hivyo inapendekezwa misikiti iwe ya umbo la mraba au mstatili na iliyo sawa, hilo ndilo lililo bora na lenye ubora zaidi. Ama kuijenga kwa mtindo uliotajwa katika swali, sijui jambo linalofanya iwe haramu, lakini kuacha mtindo huo ni bora na afadhali zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/81)
  • Imechapishwa: 25/02/2026