Swali: Ni ipi hukumu ya kuwachinjia maiti Udhhiyah?

Jibu: Sioni kama kuna ubaya akiwachinjia. Na hapana vibaya akichinja kwa ajili ya nafsi yake, familia yake na maiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo wawili; mmoja kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wa familia yake na mwingine kwa ajili ya wale wapwekeshaji katika ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo hapana vibaya mtu akichinja Udhhiyah kwa ajili yake, familia yake katika wakeze, watoto wake na wazazi wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18858/ما-حكم-الاضحية-عن-الاموات
  • Imechapishwa: 06/06/2024