Ubora wa kuchelewesha ´Ishaa kwa anayeswali peke yake

Swali: Nimesikia kuwa kuchelewesha swalah ya ‘Ishaa kwa anayeswali peke yake ni bora. Je, hilo ni sahihi?

Jibu: Ikiwa anayeswali peke yake halazimiki kuhudhuria swalah ya mkusanyiko kwa sababu ya maradhi au mfano wake, basi kuchelewesha mpaka theluthi ya usiku ni bora, kwa sababu zimepokelewa Hadiyth Swahiyh kuhusu hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/212)
  • Imechapishwa: 25/02/2026