Uadilifu kwa aliye na mke zaidi ya mmoja katika safari

Swali: Je, ni lazima kufanya uadilifu kati ya wake wawili baina yao katika safari?

Jibu: Ni wajibu awe mwadilifu baina yao katika safari kwa maridhiano au kwa kupiga kura. Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotaka kusafiri hupiga kura kati ya wake zake, kisha husafiri na yule aliyepata kura. Lililo wajibu ni kumuiga katika hilo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na maneno Yake (´Azza wa Jall):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah.”[1]

Jengine ni kwa sababu kusafiri kwake na mmoja wa wake zake bila maridhiano wala kupiga kura ni dhuluma kwa yule aliyeachwa au walioachwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameharamisha dhuluma juu ya waja Wake na akaamrisha kufanya uadilifu.

[1] 33:21

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/237)
  • Imechapishwa: 21/02/2026