Swali: Tawbah ya mzinzi inakubaliwa ni mamoja amekwishawahi kuingia ndani ya ndoa au bado hajawahi kuingia?

Jibu: Akitubu baina yake yeye na Allaah inatosha. Kuhusu upande wa adhabu anatekelezewa adhabu ya kidini pale inapothibiti kwake. Inatosha endapo atatubu, akaisitiri nafsi yake, asende kwa watawala na asiseme kitu. Katika hali hiyo haitakiwi kujifedhehesha nafsi yake. Akitambua kosa lake basi analazimika kutubia kwa Allaah baina yake yeye na Allaah. Katika hali hiyo hapana shaka kumwendea yeyote. Bali aisitiri nafsi yake na amwombe msamaha Mola wake. Inatosha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24405/هل-يقام-الحد-على-من-تاب-من-الزنا
  • Imechapishwa: 07/10/2024