Swali: Kuumikwa ni nini na ni ipi hukumu yake? Je, kuumikwa kunachengua wudhuu´ na kumfunguza mwenye swawm?

Jibu: Kuumikwa ni aina ya tiba, nayo ni kutoa damu kwa kutumia kifaa maalum cha kunyonya damu.

Kuumikwa humfunguza mwenye kufunga kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni, kwa sababu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

Kwa hiyo kuumikwa humfunguza mwenye kufunga kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni kutokana na Hadiyth hii na nyinginezo.

Vilevile kunachengua wudhuu´ ikiwa damu iliyotoka ni nyingi.

[1] Abu Daawuud (2367) na Ibn Maajah (1680).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmu´-ul-Fataawaa (2/399)
  • Imechapishwa: 18/02/2026