Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mtoto wa kike bila mtandio?
Jibu: Ikiwa hajabaleghe, basi swalah yake ni sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah hakubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa kwa mtandio.”
Hilo likajulisha kwamba asiye na hedhi – naye ni ambaye hajabaleghe – hapana ubaya kwake kuswali bila mtandio. Lakini kuswali kwake akiwa na mtandio ni bora na kamilifu zaidi ikiwa ana miaka saba au zaidi. Ama aliye chini ya miaka saba miongoni mwa wavulana na wasichana, hao si katika watu ambao swalah inawahusu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/202)
- Imechapishwa: 24/02/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mtoto wa kike bila mtandio?
Jibu: Ikiwa hajabaleghe, basi swalah yake ni sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah hakubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa kwa mtandio.”
Hilo likajulisha kwamba asiye na hedhi – naye ni ambaye hajabaleghe – hapana ubaya kwake kuswali bila mtandio. Lakini kuswali kwake akiwa na mtandio ni bora na kamilifu zaidi ikiwa ana miaka saba au zaidi. Ama aliye chini ya miaka saba miongoni mwa wavulana na wasichana, hao si katika watu ambao swalah inawahusu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/202)
Imechapishwa: 24/02/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-mtoto-wa-kike-bila-mtandio/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket