Swalah ya mchinjaji akiwa na damu

Swali: Mtu akichinja Udhhiyah na damu ikampata, je, damu hiyo ni twahara kiasi kwamba inajuzu kwake kuswali akiwa nayo kwenye nguo yake? Je, kuna tofauti katika unajisi baina ya damu inayotoka kwa wingi wakati wa kuchinja na damu iliyopo wakati wa kuchuna ngozi?

Jibu: Ikiwa damu iliyompata ni damu inayomwagika wakati wa kuchinja, basi ni najisi na ni lazima ioshwe. Hilo ni kutokana na maneno Yake (Ta´ala):

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ

“Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahy kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu [mzoga] au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe – kwani hiyo ni uchafu au ufasiki, kimechinjwa kwa ajili ya asiye Allaah.” (06:145)

Lakini ikiwa damu iliyompata ni ile inayotoka kwenye mishipa na nyama, basi ni twahara. Inasamehewa ikiwa ni tone dogo. Lakini ni vizuri kujiepusha nayo. Ama ikiwa aliswali hali ya kuwa hajui kwamba damu hiyo ipo, basi swalah yake ni sahihi.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 30/09/2026