Swali: Katika miaka iliyopita watu wa vijiji vyetu miongoni mwa wanawake walikusanyika na wakaswali swalah na ´iyd mbili kwa ukamilifu na aliwaongoza mwanamke mwenye elimu. Sababu ya kukusanyika kwao ni kwamba kiwanja cha ´iyd cha wanaume kiko mbali, unakadiriwa masaa mawili kwa kutembea kwa miguu na pia kwa sababu wanaume hawawaruhusu kwenda huko. Ni ipi hukumu ya yale waliyoyafanya wanawake hao? Je, hilo ni katika Bid´ah?

Jibu: Sijui katika hilo ubaya wowote, kwa sababu swalah ya ´iyd imewekwa katika Shari´ah kwa wanaume na wanawake. Sunnah ni kutoka kwenda kuiswali uwanjani. Ikiwa haikuwezekana kwa wanawake kutoka mpaka wakaswali pamoja na wanaume, basi waswali katika nyumba zao mmoja mmoja au kwa mkusanyiko, hapana neno katika hilo. Nao wana malipo makubwa katika hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/277)
  • Imechapishwa: 21/02/2026