Swali: Ikiwa mtu ana shaka juu ya imamu wa msikiti kwamba amefanya zinaa na wengi wa wanaoswali wanajua hilo – Je, swalah zao ni sahihi au hapana?
Jibu: Swalah zao ni sahihi, hata kama wanajua kuwa amefanya uzinzi. Maasi hayabatilishi swalah. Haya hivyo wanapaswa kumnasihi na kumuelekeza katika kheri. Pia wanapaswa kuwaomba wasimamizi wa msikiti au wenye dhamana yake wamtafute imamu mwema, iwapo huyu anatuhumiwa kwa zinaa au anajulikana kwa hilo. Ikiwa ametubia, basi jambo lake ni kati yake na Allaah. Lakini ikiwa hali yake ni mbaya, basi waswaliji msikitini wanatakiwa kumuomba msimamizi wa msikiti abadilishe imamu huyo kwa imamu mwema zaidi. Kuhusu swalah zao ni sahihi. Pamoja na hivyo wajibu wao ni kumnasihi, kumwelekeza kwenye kheri na kumtaka atubie.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1460/حكم-الصلاة-خلف-مرتكب-الزنا
- Imechapishwa: 03/04/2026
Swali: Ikiwa mtu ana shaka juu ya imamu wa msikiti kwamba amefanya zinaa na wengi wa wanaoswali wanajua hilo – Je, swalah zao ni sahihi au hapana?
Jibu: Swalah zao ni sahihi, hata kama wanajua kuwa amefanya uzinzi. Maasi hayabatilishi swalah. Haya hivyo wanapaswa kumnasihi na kumuelekeza katika kheri. Pia wanapaswa kuwaomba wasimamizi wa msikiti au wenye dhamana yake wamtafute imamu mwema, iwapo huyu anatuhumiwa kwa zinaa au anajulikana kwa hilo. Ikiwa ametubia, basi jambo lake ni kati yake na Allaah. Lakini ikiwa hali yake ni mbaya, basi waswaliji msikitini wanatakiwa kumuomba msimamizi wa msikiti abadilishe imamu huyo kwa imamu mwema zaidi. Kuhusu swalah zao ni sahihi. Pamoja na hivyo wajibu wao ni kumnasihi, kumwelekeza kwenye kheri na kumtaka atubie.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1460/حكم-الصلاة-خلف-مرتكب-الزنا
Imechapishwa: 03/04/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-nyuma-ya-imamu-mzinifu/