Swali: Bora kwa mwanafunzi anayeanza kujifunza elimu ahifadhi Qur-aan au aisome peke yake?

Jibu: Bora kwa mwanafunzi ni yeye kuhifadhi Qur-aan. Qur-aan ndio msingi wa vitabu vyote na ndio kitabu chenye manufaa zaidi. Anatakiwa kuanza kuhifadhi Qur-aan. Lakini akiweza kuhifadhi Qur-aan na sambamba na hilo akahifadhi vitabu vya Hadiyth na kuketi katika darsa za wanazuoni, basi ni kheri tupu. Lakini kama hawezi kuhifadhi Qur-aan na wakati huohuo kwenda katika darsa za wanazuoni, basi tunamwambia aanze kwa Qur-aan. Kwa sababu Qur-aan ndio msingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (20 B) Muda: 03:02
  • Imechapishwa: 06/09/2021