Nini maana ya kupinduka kwa jua (الزوال)?

Swali: Ni nini maana ya kupinduka jua (الزوال)? Lini unaanza wakati wake? Nini maana ya kivuli cha kila kitu kuwa mfano wake au mara mbili yake?

Jibu: Maana yake ni kupinduka kwa jua kuelekea upande wa magharibi. Hiyo ndio maana yake. Likielekea upande wa magharibi kwa mtazamo wa anayetazama, ndio kusudio. Hujulikana kwa vitu vilivyosimamishwa; kitu kinaposimamishwa huonekana kivuli cha kupinduka. Jua linapozama kutoka katikati na linapopinduka, kivuli huongezeka baada ya kupinduka kuelekea magharibi, hiyo ndio maana yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/205)
  • Imechapishwa: 25/02/2026