Swali: Ni lini inakuwa ni wajibu kutekeleza nadhiri? Ni lini mtu anakuwa na uchaguzi baina ya kuitekeleza na kutoa kafara?
Jibu: Inakuwa ni wajibu kutekeleza nadhiri ikiwa ni utiifu, kwa sababu ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yule mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi na amtii.”
Ikiwa ni maasi, basi ni haramu kuitekeleza na ni juu yake kutoa kafara ya kiapo.
Imekuja katika baadhi ya Hadiyth – cheni zake za wapokezi zinahitaji kujadiliwa – kwamba anapewa uchaguzi baina ya kutekeleza nadhiri na kafara ya kiapo ikiwa nadhiri hiyo ni jambo linaloruhusiwa. Kwa msemo mwingine akiweka nadhiri kwa mfano ya kupanda gari, akiweka nadhiri ya kula chakula kinachoruhusiwa au akaweka nadhiri ya kwenda matembezini, basi anapewa uchaguzi baina ya kwenda matembezini na kutoa kafara ya kiapo au kupanda gari na kutoa kafara ya kiapo. Kwa hiyo akiweka nadhiri juu ya jambo linaloruhusiwa, basi anapewa uchaguzi baina ya kulifanya na kutoa kafara ya kiapo.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
- Imechapishwa: 10/10/2026
Swali: Ni lini inakuwa ni wajibu kutekeleza nadhiri? Ni lini mtu anakuwa na uchaguzi baina ya kuitekeleza na kutoa kafara?
Jibu: Inakuwa ni wajibu kutekeleza nadhiri ikiwa ni utiifu, kwa sababu ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yule mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi na amtii.”
Ikiwa ni maasi, basi ni haramu kuitekeleza na ni juu yake kutoa kafara ya kiapo.
Imekuja katika baadhi ya Hadiyth – cheni zake za wapokezi zinahitaji kujadiliwa – kwamba anapewa uchaguzi baina ya kutekeleza nadhiri na kafara ya kiapo ikiwa nadhiri hiyo ni jambo linaloruhusiwa. Kwa msemo mwingine akiweka nadhiri kwa mfano ya kupanda gari, akiweka nadhiri ya kula chakula kinachoruhusiwa au akaweka nadhiri ya kwenda matembezini, basi anapewa uchaguzi baina ya kwenda matembezini na kutoa kafara ya kiapo au kupanda gari na kutoa kafara ya kiapo. Kwa hiyo akiweka nadhiri juu ya jambo linaloruhusiwa, basi anapewa uchaguzi baina ya kulifanya na kutoa kafara ya kiapo.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lini-mtu-anapewa-khiyari-ya-kutekeleza-nadhiri-na-kutoa-kafara/