Swali: Imekuja katika fatwa ya ”Nuur ‘alaad-Darb” ya kwamba mtu aliyeoa hali ya kuwa haswali, kisha akaongoka na akaanza kuswali ni lazima afanye upya mkataba wa ndoa. Tunaomba mtufafanulie hilo kwa undani?
Jibu: Ikiwa mke ni muislamu na yeye mume haswali, basi huyo ni kafiri. Haisihi kwa kafiri kumuoa mwanamke muislamu. Wajibu ni kufanya upya mkataba wa ndoa, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ
”Wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.”[1]
Kwa hiyo wafanye upya ndoa ikiwa mwanamke anamtaka na yeye anamtaka. Wafanye mkataba mpya kwa mahari itakayowezekana mbele ya mashahidi wawili. Walii atasema: “Nimekuoza” na mume aitikie: “Nimekubali” hata kama hawakwenda kwa mwenye kusimamia ndoa. Hata wakifanya baina yao, inatosha. Kwa sababu kusudio ni kuhalalisha ndoa kwa njia ya Kishari´ah. Kwa hiyo ikiwa walii atasema: “Nimekuoza” na mwanamke ameridhia na mume akaitikia: “Nimekubali” kwa mahari yoyote hata ikiwa ni kidogo, mbele ya mashahidi wawili, basi hilo linatosha.
[1] 60:10
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3284/تجديد-عقد-الزواج-لمن-ترك-الصلاة-ثم-تاب-من-ذلك
- Imechapishwa: 04/11/2026
Swali: Imekuja katika fatwa ya ”Nuur ‘alaad-Darb” ya kwamba mtu aliyeoa hali ya kuwa haswali, kisha akaongoka na akaanza kuswali ni lazima afanye upya mkataba wa ndoa. Tunaomba mtufafanulie hilo kwa undani?
Jibu: Ikiwa mke ni muislamu na yeye mume haswali, basi huyo ni kafiri. Haisihi kwa kafiri kumuoa mwanamke muislamu. Wajibu ni kufanya upya mkataba wa ndoa, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ
”Wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.”[1]
Kwa hiyo wafanye upya ndoa ikiwa mwanamke anamtaka na yeye anamtaka. Wafanye mkataba mpya kwa mahari itakayowezekana mbele ya mashahidi wawili. Walii atasema: “Nimekuoza” na mume aitikie: “Nimekubali” hata kama hawakwenda kwa mwenye kusimamia ndoa. Hata wakifanya baina yao, inatosha. Kwa sababu kusudio ni kuhalalisha ndoa kwa njia ya Kishari´ah. Kwa hiyo ikiwa walii atasema: “Nimekuoza” na mwanamke ameridhia na mume akaitikia: “Nimekubali” kwa mahari yoyote hata ikiwa ni kidogo, mbele ya mashahidi wawili, basi hilo linatosha.
[1] 60:10
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3284/تجديد-عقد-الزواج-لمن-ترك-الصلاة-ثم-تاب-من-ذلك
Imechapishwa: 04/11/2026
https://firqatunnajia.com/ndoa-mpya-ya-wasioswali/