Mwanamke aliye pekee amefariki kati ya wanamme wengi

189- Baba yangu amenihadithia: ´Umar bin ´Aliy al-Muqaddamiy amenihadithia: Nilimsikia Ismaa´iyl bin Hammaad akieleza kwamba baba yake aliulizwa juu ya mwanamke aliye pekee ambaye kafariki kati ya wanamme wengi. Akajibu:

“Afanyiwe Tayammum. Ambaye atabeba jukumu hilo avishe mkono wake kitambara, apige udongoni na amfanyie Tayammum.”

Nimemsikia baba yangu akisema:

“Nami naonelea hali kadhalika.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/144)
  • Imechapishwa: 26/03/2021