Muislamu anayekufa na si mswaliji haombewi rehema wala du´aa

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kufa ilihali haswali pamoja na kuzingatia kwamba wazazi wake wawili ni waislamu? Ni vipi mtu ataamiliana naye upande wa kumuosha, kumvika sanda, kumswalia, kumswalia, kumzika, kumuombea du´aa na kumtakia rehema?

Jibu: Mwenye kufa miongoni mwa wale ambao ´ibaadah ni yenye kuwawajibikia ilihali haswali ni kafiri. Kwa ajili hiyo hatooshwa, hatoswaliwa, hatozikwa kwenye makaburi ya waislamu na wala hatorithiwa na ndugu zake. Bali mali yake itaenda katika wizara ya fedha ya waislamu kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Baina ya mtu na shirki na kufuru ni kuacha swalah.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

“Ahadi ilioko baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa “as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh).

´Abdullaah bin Shaqiyq al-´Uqayliy (Rahimahu Allaah), ambaye ni mwanafunzi wa Maswahabah mtukufu, amesema:

“Hakuna kitu ambacho Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  walikuwa wanaonelea katika matendo kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah.”

Hadiyth na mapokezi yenye maana kama hii ni nyingi. Hali hii inahusu yule mwenye kuacha kwa uvivu na si kwamba anaipinga. Kuhusu yule mwenye kuiacha hali ya kuipinga ni kafiri na ni mwenye kuritadi kutoka nje ya Uislamu kwa mujibu wa wanachuoni wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/250) https://binbaz.org.sa/fatwas/3870/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D9%88%D9%87%D9%88-%D9%84%D8%A7-%D9%8A%D8%B5%D9%84%D9%8A
  • Imechapishwa: 04/01/2020