Muhrim ametokwa na madhiy baada ya kukumbatiana na kubusiana na mke wake

Swali: Mtu aliyefanya mambo ya kimapenzi hali ya kuwa yuko kwenye Ihraam, lakini hakutoa manii, bali alitokwa na madhiy. Je, kuna jambo lolote linalompasa?

Jibu: Ikiwa alifanya mambo ya kimapenzi na mke wake kisha akatokwa na madhiy, basi anawajibika kutoa fidia ya kuchinja kondoo mmoja. Wanazuoni wengi wametaja kuwa anapasa kutoa kondoo mmoja. Baadhi yao wametaja kuwa yuko na khiyari; kati ya kuchinja kondoo mmoja, kufunga siku tatu au kuwalisha masikini sita. Lakini iliyo ya tahadhari zaidi ni kuchinja kondoo mmoja, kwa sababu wanazuoni wengi wameeleza wazi kuwa anayefanya mambo ya kiromantiki na mke wake au akatokwa na madhiy, basi juu yake ni kondoo mmoja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1381/ما-يلزم-المحرم-اذا-امذى-بسبب-المباشرة
  • Imechapishwa: 05/04/2026