Swali: Ikiwa mwanaume yuko safarini ambapo akapita kwa watu wa kijiji fulani na akataka kuwaswalisha swalah ya ijumaa, kwa sababu katika kijiji hicho hakuna Khatwiyb au msafiri huyo ana elimu zaidi kuliko mkazi. Je, inajuzu kwa msafiri kutoa Khutbah na kuwaswalisha?
Jibu: Hakuna tatizo katika hilo. Wanazuoni wametofautiana kuhusu jambo hili. Baadhi ya wanzuoni wamekataa kufanya hivo, kwa sababu msafiri si wajibu juu yake ijumaa. Lakini lililo sahihi ni kwamba hakuna tatizo wala kizuizi ikiwa atawaswalisha, kwa sababu yeye kwa kimsingi ni miongoni mwa wanaolengwa na amri ya ijumaa anapokuwepo miongoni mwao na kuswali pamoja nao. Baadhi ya wanazuoni wengine wanaona kwamba ni wajibu juu yake kuswali pamoja nao anapokuwepo na ijumaa inakuwa ni wajibu juu yake kama wengine. Kwa hali yoyote ile kuondolewa wajibu wa ijumaa kwake ni kwa wepesi na kurahisisha kutokana na safari, lakini hilo halimzuii kuwaswalisha wala kutoa Khutbah ya ijumaa. Hakuna tatizo katika hilo kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi zaidi miongoni mwa maono ya wanazuoni.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1498/حكم-امامة-المسافر-للمقيمين-في-الجمعة
- Imechapishwa: 03/04/2026
Swali: Ikiwa mwanaume yuko safarini ambapo akapita kwa watu wa kijiji fulani na akataka kuwaswalisha swalah ya ijumaa, kwa sababu katika kijiji hicho hakuna Khatwiyb au msafiri huyo ana elimu zaidi kuliko mkazi. Je, inajuzu kwa msafiri kutoa Khutbah na kuwaswalisha?
Jibu: Hakuna tatizo katika hilo. Wanazuoni wametofautiana kuhusu jambo hili. Baadhi ya wanzuoni wamekataa kufanya hivo, kwa sababu msafiri si wajibu juu yake ijumaa. Lakini lililo sahihi ni kwamba hakuna tatizo wala kizuizi ikiwa atawaswalisha, kwa sababu yeye kwa kimsingi ni miongoni mwa wanaolengwa na amri ya ijumaa anapokuwepo miongoni mwao na kuswali pamoja nao. Baadhi ya wanazuoni wengine wanaona kwamba ni wajibu juu yake kuswali pamoja nao anapokuwepo na ijumaa inakuwa ni wajibu juu yake kama wengine. Kwa hali yoyote ile kuondolewa wajibu wa ijumaa kwake ni kwa wepesi na kurahisisha kutokana na safari, lakini hilo halimzuii kuwaswalisha wala kutoa Khutbah ya ijumaa. Hakuna tatizo katika hilo kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi zaidi miongoni mwa maono ya wanazuoni.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1498/حكم-امامة-المسافر-للمقيمين-في-الجمعة
Imechapishwa: 03/04/2026
https://firqatunnajia.com/msafiri-anataka-kuwaswalisha-ijumaa-wakazi-wa-kijiji/