Swali: Ninaye babu mwenye umri mkubwa na watoto wake hawawezi kuhiji kwa niaba yake, naye ni mgonjwa na mzee. Je, inajuzu kwa mimi, ambaye ni mpwa wake, kuhiji kwa niaba yake na kwa niaba ya bibi yangu, pamoja na kuzingatia kwamba bibi yangu ameshafariki?
Jibu: Umefanya vizuri, hapana vibaya kuhiji kwa niaba yake. Allaah akujaze kheri. Hili ni miongoni mwa kuunga kizazi na ni katika wema. Ikiwa ni mgonjwa kwa magonjwa yasiyotarajiwa kupona au ni mzee asiyeweza, muhijie. Hukumu hiyohiyo inamuhusu maiti. Hili ni miongoni mwa wema na kuunga kizazi. Wewe ni mwenye kushukuriwa na kupata ujira. Alikuja mwanamke mmoja akasema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu ni mzee mkubwa ambaye hawezi kuhiji wala kusafiri. Je, nihiji kwa niaba yake?” Akasema: ”Hiji kwa niaba ya baba yako.”
Wakati mwingine kuna mwanaume mmoja alikuja na kusema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu ni mzee mkubwa anbaye hawezi kukaa juu ya kipando. Je, nihiji kwa niaba yake na nimfanyie ´Umrah?” Akasema: ”Hiji kwa niaba ya baba yako na mfanyie ´Umrah.”
Kwa hiyo ukihiji kwa niaba ya babu yako, bibi yako, wengineo miongoni mwa wafu au wazee wasio na uwezo, hapana vibaay. Kadhalika inapokuja katika jambo la ´Umrah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30941/هل-يجوز-لابن-البنت-الحج-عن-جده-المريض
- Imechapishwa: 13/09/2025
Swali: Ninaye babu mwenye umri mkubwa na watoto wake hawawezi kuhiji kwa niaba yake, naye ni mgonjwa na mzee. Je, inajuzu kwa mimi, ambaye ni mpwa wake, kuhiji kwa niaba yake na kwa niaba ya bibi yangu, pamoja na kuzingatia kwamba bibi yangu ameshafariki?
Jibu: Umefanya vizuri, hapana vibaya kuhiji kwa niaba yake. Allaah akujaze kheri. Hili ni miongoni mwa kuunga kizazi na ni katika wema. Ikiwa ni mgonjwa kwa magonjwa yasiyotarajiwa kupona au ni mzee asiyeweza, muhijie. Hukumu hiyohiyo inamuhusu maiti. Hili ni miongoni mwa wema na kuunga kizazi. Wewe ni mwenye kushukuriwa na kupata ujira. Alikuja mwanamke mmoja akasema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu ni mzee mkubwa ambaye hawezi kuhiji wala kusafiri. Je, nihiji kwa niaba yake?” Akasema: ”Hiji kwa niaba ya baba yako.”
Wakati mwingine kuna mwanaume mmoja alikuja na kusema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu ni mzee mkubwa anbaye hawezi kukaa juu ya kipando. Je, nihiji kwa niaba yake na nimfanyie ´Umrah?” Akasema: ”Hiji kwa niaba ya baba yako na mfanyie ´Umrah.”
Kwa hiyo ukihiji kwa niaba ya babu yako, bibi yako, wengineo miongoni mwa wafu au wazee wasio na uwezo, hapana vibaay. Kadhalika inapokuja katika jambo la ´Umrah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30941/هل-يجوز-لابن-البنت-الحج-عن-جده-المريض
Imechapishwa: 13/09/2025
https://firqatunnajia.com/mpwa-anataka-kumhijia-babu-na-bibi-yake/