Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliyeota akamwaga manii mchana wa swawm? Je, hilo linaathiri usahihi wa swawm yake?

Jibu: Mwenye kupata ndoto ya janaba mchana wa swawm, ni wajibu kwake kuoga josho la janaba. Ama kuhusu swawm yake ni sahihi, kwa sababu ndoto ya janaba hutokea bila kutaka kwake na bila kukusudia; yamemtokea bila kutaka kwake. Kwa hivyo hayaathiri swawm yake. Swawm yake ni sahihi na haina kasoro. Lakini ni wajibu kwa muislamu anapopata ndoto ya janaba akiwa amefunga na akamwaga manii, aoge josho la janaba.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/403-404)
  • Imechapishwa: 18/02/2026