Matendo ya mwenye kuritadi baada ya tawbah

Swali: Mja akitubia matendo yake yanarudi kwake baada ya tawbah?

Jibu: Mja akitubia matendo yake yaliyotangulia yanarudi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Umesilimu juu ya zile kheri zilizotangulia.”[1]

Matendo yake hayakatiki isipokuwa akifa juu ya ukafiri. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ

“Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri.”[2]

Akifa juu ya ukafiri matendo yake yanakatika. Vinginevyo abaki juu ya uongofu. Kwa sababu amesilimu na akaongozwa na Allaah.

Swali: Je, matendo yake yanapotea akifa hali ya kuwa ni murtadi?

Jibu: Kinaharibika kila kitu. Akifa juu ya kuritadi kinapotea kila kitu. Amesema (Ta´ala):

قَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا

”Tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo, Tutayafanya kuwa ni vumbi lililotawanyika.”[3]

[1] Muslim (123).

[2] 04:18

[3] 25:23

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 105
  • Imechapishwa: 13/08/2019