Maoni ya wanazuoni wengi kuhusu swalah ya mwanamke miguu wazi

Swali: Wanawake wengi wanaswali hali miguu yao iko wazi. Baadhi ya watu wanawaambia kuwa hilo halina tatizo?

Jibu: Kwa hali yoyote ile ni lazima ijulikane kwamba kufunika miguu kwa mujibu wa kikosi kikubwa cha wanazuoni ni wajibu, kwa sababu miguu ni uchi. Baadhi ya wanazuoni, kama Abu Haniyfah na kundi jingine, wanasema kuwa miguu si uchi, na kwa sababu hiyo baadhi ya watu wanafanyia kazi maoni haya. Lakini sahihi ni kwamba miguu ni uchi. Kilichobaguliwa ni uso tu. Vilevile mikono kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu zaidi katika swalah si uchi. Ama mwili wake, kichwa chake na mwili wake wote, kukiwemo miguu yote, ni uchi ndani ya swalah. Hii ni kwa mujibu wa mtazamo wa wanazuoni wengi. Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa miguu si uchi, kama Abu Haniyfah na wengine. Lakini inampasa mwanamke kufunika miguu yake pia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1467/حكم-صلاة-المراة-كاشفة-لرجليها
  • Imechapishwa: 03/04/2026