Swali: Nilifanya dhambi katika Ramadhaan. Je, inaharibu swawm yangu au hapana?

Jibu: Hatujui ni dhambi ipi kama inaharibu swawm au hapana. Dhambi hii ikiwa inaharibu swawm, basi swawm yake imeharibika.

Tumetaja mambo yanayoharibu swawm katika darsa. Hata hivyo ikiwa ni maasi yasiyokuwa na uhusiano wowote na [kuharibika kwa] swawm, hayaiharibu swawm. Mfano wa hilo ni mtu akawasengenya ndugu zake waislamu mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga. Hii ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa, lakini pamoja na hivyo haiharibu swawm. Bali inaipunguza swawm.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 03
  • Imechapishwa: 23/09/2020