Maafikiano ya wanazuoni juu ya uharamu wa miraa

Vivyo hivyo miraa inayojulikana Yemen na katika nchi nyingine ndani yake kuna kulevya, kulewesha katika baadhi ya nyakati na uharibifu kwa mwili na viungo. Ndani yake kuna shari nyingi. Kwa sababu hiyo wanaoijua vizuri wameamua kuiharamisha. Ulifanyika mkutano wa Kiislamu Madiyna na maoni ya waliohudhuria mkutano miongoni mwa wanazuoni walitoa maafikiano juu ya kuharamishwa kwa miraa na sigara, kwa sababu ya madhara mengi waliyoyajua yaliyomo ndani yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2240/حكم-الدخان-والمسكرات-والقات-وحكم-امامة-من-يشربها
  • Imechapishwa: 05/03/2026