Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ

“Wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu na wanawake wasiopata hedhi [ni vivo hivyo].”[1]

Aayah hii inawaraddi wale wenye kupinga ndoa za watoto wa kike wenye umri mdogo? 47

Jibu: Ndio:

وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ

“… wanawake wasiopata hedhi [ni vivo hivyo].”

Inalenga watoto wa kike wenye umri mdogo. Hawajapata hedhi kwa sababu ya udogo. Hii ni Radd ya wazi. Ni kina nani wanaopinga ndoa watoto wa kike wenye umri mdogo? Wanapingana na hukumu za Allaah? Anafanya hivo kwa sababu ya matamanio na ujinga? Haijuzu. Ni upotevu. Ni nani anayekataza kuwaozesha watoto wa kike wenye umri mdogo? Anakataza hukumu ya Kishari´ah? Ana dalili gani juu ya hilo? Hili si jengine isipokuwa ni mfano wa kujikakama kwao na kupingana na hukumu za Shari´ah. Wanataka kuwa na huruma kwa wasichana wenye umri mdogo? Baba yake ana huruma zaidi kuliko wao. Akiwepo baba anayetaka kumuozesha msichana wake kwa sababu ya maslahi yake binafsi, anatakiwa kukatazwa. Hali kama hizi si mara nyingi kupatikana. Ama kukataza kuwaozesha wasichana wenye umri mdogo kabisa kabisa ni kuwa na ujasiri wa kushambulia hukumu za Allaah na haijuzu. Ikiwa inahusiana na mchezo, jambo hilo likatazwe. Hili linahusiana hata na mwanamke mtumzima.

[1] 65:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 17/12/2016