Swali: Muulizaji kutoka Ubelgiji anauliza kwa kusema kwamba pindi anapofariki muislamu wanamsafirisha maiti kwenda katika nchi yake ili azikwe huko kwenye makaburi ya waislamu. Lakini kanuni katika nchi zao zinashurutisha maiti azikwe ndani ya sanduku la chuma lililofungwa na anazikwa ndani ya sanduku hilo. Je, kutokana na sababu hiyo imechukizwa kumzika maiti ndani ya sanduku la chuma?

Jibu: Wasiwakubalie kumzika ndani ya sanduku. Wasiwatii. Kumuweka ndani ya sanduku wakati wa kumpeleka hakuna neno. Ama kumzika ndani ya sanduku hilo hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 29/08/2020